SHARUMA inaunganisha namba yako ya WhatsApp na AI ya Kiswahili, kampeni na inbox ya timu yako. Wateja wanapata majibu papo kwa papo; wewe unapata oda, taarifa na muda wa kufanya kazi nyingine.
Hakuna kadi ya benki kuanza · Inaendana na Meta WhatsApp Cloud API · AI inaweza kukabidhi mtu wakati wowote.
Badala ya kutumia apps tano, tumia jukwaa moja: majibu, mauzo, kampeni na ripoti.
Inajibu maswali ya kawaida, inaelekeza kwenye bidhaa au huduma, na inamkabidhi mtu wako pale inapohitajika.
Tuma ujumbe kwa wateja waliokubali, kwa template zilizoidhinishwa na Meta, na uone waliofungua na waliojibu.
Mazungumzo yote mahali pamoja. Mfanyakazi anaweza kuchukua mazungumzo, na AI inanyamaza mara moja.
Bidhaa, bei, kikapu, oda na uthibitisho wa malipo — mtandaoni na ndani ya WhatsApp.
Muda wa kujibu, maswali yanayorudiwa, mauzo na utendaji wa kampeni — kwa lugha rahisi.
Kila mteja ana data yake pekee. Tokeni zimesimbwa, na mteja anaweza kuzuia ujumbe (opt-out) wakati wowote.
Weka taarifa za biashara na chagua mpango. Siku 14 za majaribio zinaanza mara moja.
Unganisha namba kwa Meta Cloud API (rasmi) au QR ya haraka kwa namba ya kawaida.
Ongeza bidhaa/huduma, bei, saa za kazi na maswali yanayorudiwa — AI itajifunza hapo.
AI inajibu, timu inachukua inapohitajika, na wewe unaona ripoti kila siku.
Chagua mpango unaokufaa. Unaweza kubadilisha au kuacha wakati wowote.
Bei ni kwa mwezi na haijajumuisha VAT. Unaweza kubadilisha au kuacha mpango wakati wowote.
Kuanza majaribio ya SHARUMA hakuhitaji kadi. Kwa namba rasmi ya Meta Cloud API, Meta inahitaji njia ya malipo kwenye akaunti yako ya WhatsApp baada ya ujumbe 1,000 wa huduma bure kwa mwezi. Kama huna kadi, unaweza kuanza kwa QR (Evolution) au tukuwasiliane.
AI inajibu kwa kutumia taarifa ulizozithibitisha tu (bidhaa, bei, saa, sera). Inaweza kukabidhi mazungumzo kwa mtu wako pale inapokuwa haijui jibu, na mtu anaweza kuchukua mazungumzo wakati wowote.
Meta Cloud API ni njia rasmi na salama. Ikiwa unatumia QR (Evolution), ni njia isiyo rasmi — inafaa kwa kuanza, lakini kwa kampeni kubwa tunapendekeza Cloud API.
Ndiyo. Unaweza kupanda au kushuka mpango wakati wowote; mabadiliko yanafanyika kwenye kipindi kinachofuata cha malipo.
Hapana. Bei iliyoonyeshwa ni ya mwezi bila VAT. Ankara/risiti zitakazotolewa zitaeleza kodi kwa mujibu wa sheria.
Ndiyo. Timu yetu inakusaidia kuhakiki biashara, kuunganisha namba na kupitisha template za ujumbe. Unaweza kuanza mwenyewe kwa Embedded Signup ndani ya dashibodi.
Anza bure leo; ongeza timu na kampeni baadaye.